Serikali imezitaka
wizara mbalimbali kuhakikisha zinahamishia makazi yake Makao Makuu ya nchi
mkoani Dodoma kabla ya Februari 28, mwaka huu, kama iliyotangazwa na Rais John
Magufuli mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Ulemavu, Jenista Mhagama, amesema
agizo la serikali lazima liwe limetekelezwa ifikapo Februari 28, mwaka huu.
Waziri Mhagama amesema ofisi yake imeweza kukagua miundombinu na
ujenzi wa majengo mbalimbali ya serikali yanayoendelea kujengwa na mengine
yakiwa yamekamilika kwa ajili ya matumizi ya wizara hizo.
Post a Comment