0


Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi visiwani Zanzibar, Ayoub Mohamed amesema Serikali  inaendelea kuimarisha hali ya usalama barabarani kwa kutumia njia za teknolojia ili kupunguza ajali za mara kwa mara.


              Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi visiwani Zanzibar, Ayoub Mohamed

   Akipokea msaada wa ipod 13 kutoka kampuni ya simu za mkononi Zantel kusaidia mawasiliano  ya upatikanaji wa taarifa za matukio hayo amesema serikali ya mkoa wake kwa kushirikiana na jeshi la polisi inakusudia kuzindua mtandao huo ambapo vifaa hivyo vitasaidia kutoa taarifa kwa wakati na kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa haraka .

Katika hatua nyengine Mh Ayoob ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za matukio ya uvunjifu wa sheria kupitia mitandao ya simu punde mtandao huo utakapokamilika.

Nae  Naibu kamishina wa Jeshi la polisi Zanzibar DCP Juma Yussuf amesema kuwa asilimia 75 ya makosa ya barabarani husababishwa na uzembe wa madereva na watumiaji wa Barabara ambapo ameahidi kuvitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa kampuni ya Zantel Moh’d Khamis Mussa amesema gharama ya vifaa hivyo ni shilingi 20 milioni huku vikiwa vimeunganishwa vifurushi vya tatu GB

Post a Comment

 
Top