0



Waziri wa nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Tanzania Mh Angelah Kairuki amesema Zanzibar hakuna kaya masikini  hewa bali kuna upungufu wa vigezo vinavyohitajika kwa baadhi ya watu ili wakubalike kama ni kaya masikini.



  Waziri wa nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Tanzania Mh Angelah Kairuki

      Mh Kairuki ameyasema hayo katika ziara ya kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika utekelezaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF) iliyofanyika Donge visiwani Zanzibar


Amesema  kuwa wakati wa mahojiano yake na kaya masikini hakupata taarifa kwamba kuna kaya masikini hewa bali amethibitisha kwamba kuna upungufu wa vigezo vinavyostahiki mtu huyo kuitwa masikini.

Eitha Mh Kairuki ameeleza kufurahishwa na miradi mbali mbali ya wanakaya masikini walioanzishwa ambayo inatokana na fedha za TASAF ikiwemo miradi ya matunda ya kutia damu mwilini, miche ya michungwa, malimau, mishoki shoki, minazi , pamoja na mikarafuu.
Amesema fedha za TASAF ni fedha za mkopo serikali imekopa katika Bank ya Dunia na fedha hizo zinahitajika kulipwa hivyo watakozitafuna fedha hizo watachulikiwa hatua kali kwani Serikali ya Jamuhuri ya Muungano  ya Tanzania imeshaanza kuwachulia hatua watu waliofanya ubadhirifu katika fedha za TASAF.

Naye Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud amesema ni vizuri kuziendeleza jitihada ambazo wananchi wamezianzisha  hivyo ipo haja ya wataalamu nchini kukaa na kufikia soko ili wazalishaji wa ndani ya nchi waweze kuuza bidhaa zao wanazozizalish


Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud
 
Amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshapanga utaratibu wa kuanzisha ufugaji wa samaki hivyo viongozi wa TASAF iwajenge uwezo kaya masikini kuanzisha mradi huo.

Ziara ya kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika utekelezaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF) ilifanyika jana ambapo wabunge hao walijigawa nusu walikwenda Mkoa kusini Unguja na wengine kueleka Kaskazini Unguja.

Post a Comment

 
Top