NAIBU Waziri Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Usafirishaji Zanzibar Mh, Mohamed Ahmada
ameitaka kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Wete kuhakikisha vyombo vya
mizigo havitumiki kubeba abiria.
Akizungumza na viongozi hao Mhe.
Mohamed Ahmada amesema kumekuwapo na vyombo vya mizigo vinavyojihusisha na
kubeba abiria kupitia bandari ya Wete na bandari nyengine bubu kwenda mkoani
Tanga na Mombassa.
Amefafanua kuwa hatua hiyo inakuja baada ya kuripotiwa ajali za mara kwa
mara katika bahari ya Hindi, amesema kamati ya ulinzi na Usalama na Mamlaka ya
usafirishaji, na Serikali kuu zinawajibu wa kudhibiti vyombo
visivyoruhusiwa kuchukua abira ili visifanye kazi hiyo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid
amesema wamepokea taarifa ya ajali ya chombo cha
Sayari kwa mshtuko kwani ajali hiyo imepoteza maisha ya watu
wasiokuwa na hatia .
Mkuu wa Wilaya amefahamisha kwamba Serikali ya Wilaya imekuwa ikichukua
hatua za makusudi kuwaelimisha wananchi kuacha kutumia vyombo
vilivyosajiliwa kwa ajili ya kubeba mizigo kusafiria
Post a Comment