NB-Siyo daraja katika habari hapa chini |
MKAZI
wa kijiji cha Sakalilo kilichopo mwambao wa Ziwa Rukwa wilayani
Sumbawanga, Kalitus Jacob (44) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha
kali kisogoni kisha mwili wake ukatupwa chini ya daraja la Mumba na watu
wasiojulikana.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema tukio hilo lilitokea
Januari 16 mwaka huu, saa 12:00 jioni katika kijiji cha Sakalilo “Kabla
ya tukio, alionekana akiwa kilabuni na wake zake wawili wakinywa pombe,
aliwaaga na kuondoka na hakurudi tena hadi alipokutwa akiwa amekufa.
Chanzo
cha mauaji hakijajulikana na juhudi za Jeshi la Polisi zinaendelea ili
kubaini kiini cha mauaji hayo,” alieleza Kamanda Kyando.
Alisema
kuwa mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya
maandalizi ya maziko yake baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu.
Alisema watuhumiwa hawajakamatwa huku uchunguzi unaendelea ili kuweza kuwabaini waliohusika katika mauaji hayo.
IMEANDIKWA NA PETI SIYAME,-HABARILEO SUMBAWANGA
Post a Comment