0

 Mkuu wa wilaya ya Liwale,Mhe Sarah Chiwamba akizungumza na waendesha pikipiki,bajaji na tax kwenye mkutano uliofanyika januari 07 mwaka 2017 kwenye ofisi ya chama cha bodaboda wilayani Liwale mkoani Lindi.

 Madereva wa bodaboda wakiwa kwenye mkutano na mkuu wa wilaya ya Liwlae uliofanyika januari 7 mwaka 2017
 Madereva wa bodaboda wakiwa kwenye mkutano na mkuu wa wilaya ya Liwlae uliofanyika januari 7 mwaka 2017

Mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe.Sarah Chiwamba mkoani Lindi amewataka na kuwakumbusha  madereva wa vyombo vya moto wilayani  kufuata sheria za barabarani ili kupunguza ajali zinazosababishwa na uzembe.

Hayo aliyasema januari 07 mwaka 2017 kwenye mkutano na madereva wa vyombo vya moto kwenye ofisi ya chama cha waendesha  pikipiki,bajaji  na tax (bodaboda) iliyopo kata ya Liwale mjini wilayani hapa.

"Tumeanza mwaka 2017 tuanze na mwaka huu kwa nguvu kabisa kwamba vifo na majeraha yoyote yanayosababishwa na uendeshaji mbovu wa vyombo vya moto tunakomesha kabisha"alisema Chiwamba

Chiwamba amesema bodaboda zilikuja kwa lengo la kujikwamua kiuchumi lakini sasa imekuwa tatizo kubwa kutokana na uendeshaji mbovu ambao unaosababisha ajali nyingi na kupelekea watu wanakufa na kuwasababisha vilema.

Mkuu wa wilaya asisitiza maderevya wa pikipiki hao kuvyaa kofia ngumu na kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za barabarani pia aliongeza kusema licha ya kufanya shughuli ya bodaboda aliwaomba kuongeza shughuli za ujasiliamali ili kuweza kuongeza kipata.
Kwa upande wake mkuu wa usalama barabarani wilayani hapa,Godson Lucas Majogo asisitiza madereva kuvaa kofia ngumu na kuwataka madereva hao kuacha kubeba abilia wawili maalufu kama mishikaki huku akisema moja ya athali za kubeba watu wawili kutokea kwa uhalifu.
Picha ya pamoja kati ya mkuu wa wilaya ya Liwale,viongozi mbalimbali  pamoja na madereva wa vyombo vya moto. (Picha na Liwale Blog)

Post a Comment

 
Top