Lindi. Zaidi ya vijana 250 wa mikoa ya Lindi na Mtwara, wanatarajia
kupata ajira baada madini aina ya Bunyu (Kinywe) kugundulika katika
vijiji vya Namangale, Utimbe, Chidya na Chiwata.
Hayo yameelezwa na Mhandisi wa Migodi Kanda ya Kusini, Aidan Mhando kwenye kongangamano la wadau wa mradi wa uchimbaji wa madini ya bunyu katika vijiji hivyo.
Mhandisi Mhando alisema uchimbaji unatarajia kuanza hivi karibuni na kwamba, hatua iliyobaki ni kupata leseni ya uchimbaji baada ya shughuli zingine kukamilika.
Baadhi ya kampuni za utafiti zilizogundua madini hayo ni Urinex Ruangwa, Nachi Jumbo na Ngwena. Akiba ya madini hayo ambayo yana rangi nyeusi yanayotumika kutengenezea vifaa vya umeme, ni tani 689.7 milioni.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, Mwakilishi wa Kampuni ya Nachi Jumbo, Mhandisi Jimmy Ijumba alisema kampuni hiyo ambayo itachimba madini hayo inatarajia kusafirisha tani 100,000 hadi 180,000 kwa mwaka.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee alitoa wito kwa wawekezaji ikiwamo Kampuni ya Nachi Jumbo kutumia uzoefu wa utekelezaji miradi iliyofanyika ili kuepuka migogoro kutokana na kutolipa fidia wananchi kwa wakati.

Post a Comment