Bodi ya usafiri wa barabarani Zanzibar imewataka wananchi kurecord namba za Gari za abiria ( Dala dala) zinazopandisha bei kiholela na kuzifikisha kwenye idara ya usafiri na leseni ili sheria ifuate mkondo wake.
Hayo yameelezwa na Katibu
wa bodi hiyo Mohamed Simba ambapo amesema hatua hiyo itasaidia wahusika wa vyombo
hivyo kutoza nauli zilizopangwa kisheria na Serikali.
Amefahamisha
kuwa dereva atakaebainika gari yake kuwatoza nauli kubwa abiria, atanyang’anywa
leseni pamoja na kuifungia gari husika kufanya biashara ya ubebaji wa abiria katika Visiwa vya Zanzibar.
Aidha
Simba amewataka madereva na makondakta kuacha kukiuka sheria zilizowekwa na
Idara ya usafiri na leseni ili kuendelea kuimarisha huduma ya usafiri nchini.
Post a Comment