Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Visiwani Zanzibar Ayoub Mohamed
amewataka wananchi kuacha kuharibu kwa makusudi miundombinu inayowekwa na
Serikali.
Kauli
ya mkuu huyo wa mkoa inakuja siku chache baada ya mtu asiyejulikana kulipasua
kwa makusudi bomba la maji huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi B, mkoa wa Mjini
magharibi Unguja.
Akizungumza
katika eneo lilipotokea tukio hilo, Mhe. Ayoub amesema uchunguzi wa awali
unaonesha kua chanzo
cha tukio hilo ni chuki
za kisiasa ambazo zimepamba moto
kutokana na kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la
Dimani.
Aidha mkuu wa mkoa amefahamisha kuwa
kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo inaendlea na uchunguzi kumpata
aliyehusika na tukio hilo huku akiwataka wale wote wanaojihusisha na vitendo
vinavyoashiria uvunjifu kuacha mara moja kabla hawajachukuliwa hatua za
kisheria.
Tayari
bomba lililoharibiwa limefanyiwa matengenezo ambapo wakazi wa eneo hilo
wameiambia wamesema kuwa upatikanaji wa huduma ya maji imerudi katika hali
yake ya kawaida.
Post a Comment