Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza
Uongozi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kuharakisha matengenezo ya Mashine ya uchunguzi
wa Maradhi ya Matumbo (Utra sound) ili kupunguza msongamano wa Wagonjwa
wanaohitaji huduma hizo.
Ametoa
agizo hilo alipofanya ziara fupi kukagua chumba cha uchunguzi wa maradhi ya
Matumbo katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ambapo Mashine moja kati ya Mbili
zilizomo ndani ya chumba hicho imeharibika kwa zaidi ya miezi miwili sasa.
Amesema
Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ndio kimbilio pekee la Wananchi wote wa
Zanzibar wanalolitegemea kukidhi mahitaji yao ya
dharura wakati wanapokumbwa na matatizo mbali mbali ya kiafya.
Ameongeza
kuwa mabadiliko ya kimaisha katika mazingira ya matumizi yasiyo sahihi ya
vyakula mchanganyiko wanavyotumiwa Wanaadamu yamechangia ongezeko la mardhi
tofauti yakiwemo yale yanayowasumbua akina Mama ya Matumbo.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dkt. Ali Salum Ali amesema juhudi za matengenezo
za Mashine hiyo tayari zimeshachukuliwa na Uongozi huo ili kuurejesha
mpangilio wa huduma hizo uwe wa kawaida.
Hata hivyo
Dr. Ali amesema kilichochelewesha kukamilika kwa matengenezo hayo ni mtaalamu
wa kuifanyia marekebisho Mashine hiyo ambaye analazimika kutoka nje ya
Zanzibar.
Post a Comment