0
Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara SIMBA imeshindwa kuibuka na point tatu katika uwanja wa Jamhuri Morogoro Baada ya kulazimishwa  sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar  katika mwendelezo wa raundi ya lala salama ya ligi Kuu Tanzania bara.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha alama 45 baada ya kucheza mechi 19 na wanakuwa mbele kwa pointi mbili tu, mabingwa watetezi, Dar es Salaam Young African. 
Kipindi cha kwanza Mtibwa Sugar walionekana kucheza kwa kujihami zaidi na kushambulia kwanafasi kubwa lango la timu ya simba

Ukuta wa Simba hii leo pia ulionekana uko makini huku Kipa wa Simba, Daniel Agyei akidaka shuti la mshambuliaji Rashid Mandawa aliyeunganisha krosi ya Henry Joseph dakika ya 8 ya mchezo huo.
Simba wakaamka katika dakika nane baadaye, ambapo kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed alidaka shuti lililopigwa na  beki wa kushoto  wa Simba Mohammed Hussein.

Simba ilipoteza nafasi nyingi katika mchezo wa leo baada ya Mavugo kupaisha juu katika dakika za 36 na 40 na kipindi cha pili akatolewa kumpisha Ibrahim Hajib Migomba.

Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa kiujumla kilikuwa ; Said Mohamed, Ally Shomary, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Henry Joseph, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Haruna Chanongo, Ally Makarani, Rashid Mandawa, Jaffary Salum/Hussein Javu dk84 na Vicent Barnabas/Kevin Friday dk78.
Simba SC; Daniel Agyei, Hamadi Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Method Mwanjali, Abdi Banda, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Jamal Mnyate dk82, James Kotei, Juma Luizio, Laudit Mavugo/Ibrahim Hajib dk54 na Mwinyi Kazimoto/Pastory Athanas dk75.


Post a Comment

 
Top