Muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC Kwa kushirikiana
na wadau wa habari wamefungua kesi kwenye mahakama kuu kanda ya Mwanza
kupinga sheria mpya ya huduma za vyombo vya habari ya mwaka 2016
Wadau hao wanadai kuwa sheria hiyo imekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 inayotoa haki na uhuru wa mtu kutoa na kupata taarifa.
Akizungumza kutoka katika mahakama hiyo mwanasheria Jebra Kambole amesema katika kesi hiyo ya kikatiba namba mbili ya mwaka 2017 inayosimamiwa na wanasheria 6 wakujitegemea imelenga kuishinikiza serikali kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungu kwenye sheria hiyo kikiwepo kifungu namba 8,35 hadi 39 na 52 hadi 59 vya sheria ya huduma za vyombo vya habari namba 12 ya mwaka 2016.
Kesi hiyo inafunguliwa ikiwa ni siku chache tangu wadau wengine wafungue kesi kwenye mahakama ya Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam huku wadau wa habari wakiendelea kutilia mgomo kushiriki mchakato wa kutunga kanuni za sheria hiyo.

Post a Comment