Takriban watu 50
wameuawa kaskazini mwa Mali wakati wa shambulizi la bomu la kutegwa
ndani ya gari lilitokea kwenye kambi ya jeshi.
Tukio hilo
lilitokea wakati gari lililokuwa limejazwa mabomu, lililipuka kwenye
kambi iliyokuwa na wanajeshi na wanachama wa makundi hasimu katika mji
wa Gao.Eneo la kaskazini mwa Mali limekumbwa na msukosuko tangu litekwe na wanamgambo wa kiislamu mwaka 2012.
Kambi iliyoshambuliwa iko Goa, ambao ni mji mkuu wa kaskazini mwa Mali.
Taarifa kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, inanukuliwa na AFP ikisema kuwa shambulizi hilo ni la kujitoa mhanga.
Waathiriwa walikuwa wakitoa huduma za kupiga doria eneo lenye msukosuko zaidi, chini ya mkataba ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kusitisha ghasia huko.
Hii si mara ya kwanza jeshi linalengwa nchini Mali.
Mwezi Julai mwaka uliopita karibu wanajeshi 17 waliuawa na wengine 30 kujeruhiwa, wakati kambi ya jeshi ilishambuliwa katika mji ulio kati kati mwa nchi wa Nampala.
Washambuliaji walichoma moto sehemu ya kambi hiyo kabla ya kukimbia.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza siku tatu za kuomboleza
Post a Comment