Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Anastazia Francis (48)
amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa katika mtaa Nyasaka wilaya ya Ilemela
jijini Mwanza.
Taarifa ya jeshi la
Polisi mkoa wa Mwanza imesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa
11:00 asubuhi, mwanamke huyo alikutwa akiwa amejinyonga hadi kufa ndani ya
chumba chake kwa kutumia mtandio ambao alikuwa ameuning’iniza kwenye dirisha.
Inadaiwa kuwa
mwanamke huyo baada ya mumewe kuondoka alimtuma mwanae mkubwa aliyemaliza
kidato cha nne aende dukani na mwingine mdogo mwenye umri wa miaka 06 aende
kufagia na ndipo alipopata mwanya wa kwenda kujinyonga hadi kufa.
Tukio
hilo lilijulikana baada ya mtoto wake mdogo kurudi ndani chumbani kuchukua
shati na kumkuta mama yake akiwa amejining’inizi ndipo aliita watu ili waje
kumsaidia.
Taarifa hiyo ya jeshi la
polisi imesema kuwa upelelezi unaendelea ili kufahamu chanzo cha tukio hilo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amewaasa wananchi pindi wanapopata
matatizo waombe ushauri kwa watu wengine ili kuweza kuepusha maamuzi ambayo ni
hatari katika maisha yao.
Post a Comment