JESHI la Polisi Zanzibar linatarajia kumfikisha mahakamani mtu anayedaiwa kumkashifu Mtume Muhammad (S.A.W).
Mtuhumiwa huyo, Dk. Abdallah Saleh Abdallah (50), mkazi wa Kikwajuni
mjini Unguja, baada ya kutoa maneno hayo ya kashfa juzi na kusambaa
kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja, Kamishna wa Jeshi la
Polisi visiwani hapa, Hamdan Omar Makame, alisema walimtia mbaroni
daktari huyo wa binadamu baada ya taarifa zake kusambaa kwenye mitandao
ya kijamii, ikiwamo wa Facebook.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkashifu Mtume Muhamad na waumini wa dini ya Kiislamu.
“Tumemkamata mtuhumiwa na tayari tumeshakamilisha kila kitu, ikiwamo
taarifa za upelelelezi. Hivyo kilichobaki ni kumfikisha makahamani tu
ili aweze kujibu mashtaka yake,” alisema Kamishna Makame.
Akiongezea kuhusu ukusanyaji wa taarifa za upelelezi, alisema
wamelazimika kumshikilia kijana Ali Juma Makame (30) mkazi wa Michenzani
mjini hapa ambaye anatuhumiwa kusambaza video hizo mitandaoni.
“Tunawanasihi waumini wa dini ya Kiislamu kutokubali kuyumbishwa na
kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria, ni
bora kujiepusha na jambo hili kwani tayari vyombo vya ulinzi
vimeshachukua hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Kutokana na video hiyo, taasisi mbalimbali za dini ikiwamo Jumuia ya
Maimamu Zanzibar (JUMAZA) na Ofisi ya Mufti, zimelaani tukio hilo na
kutoa wito vyombo vya sheria kuchukua hatua na kufanya kazi bila
upendeleo.
Chanzo-Mtanda blog
Post a Comment