0

Wadau mbalimbali wa mchezo wa bao walioudhulia kwenye ufunguzi wa tamasha la michezo leo disemba 29 wilayani Liwale  (picha na Liwale Blog)


 Ofisi ya utamaduni na michezo wilaya ya Liwale mkoani Lindi kwa kushirikiana na wadau wa michezo waliopo ndani ya wilaya ya Liwale wameandaa Tamasha la michezo mbalimbali kwa ajili ya kuuga mwa 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.

Dhumuni la tamasha hilo kuongeza kushirikiano katika jamii  na michezo huleta furaha,amani na upendo.
Kwa mujibu wa kaimu afisa utamaduni na michezo wilaya,Selemani Nangomwa amesema katika tamasha hilo itahusisha michezo kama ridha(marathoni fupi),mbio za baiskeli,bao,kukuna nazi wanaume.

Michezo ingine ni kufukuza kuku wanawake na kukimbia na ndoo ya maji kwa wanaume bila kushikiria pia kutakuwa na mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya watani wa jadi timu ya Hawili fc dhidi ya Sido fc.

Tamasha hilo limenza rasmi leo disemba 29 lililofunguliwa na kaimu afisa utamaduni na michezo Nangomwa kwa mashindano ya bao yaliyofanyika katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale.

Disemba 30 ijumaa kutakuwa na mbio za baiskeli na marathoni mbio hizo zitafanyika majira ya saa 9:30 Jioni katika barabara ya rami liwale mjini,disemba 31 jumamosi kutakuwa na mashindano ya kukuna nazi,kukimbia na ndoo kichwani na kufukuza kuku na mchezo wa fainali wa bao katika uwanja wa halmashauri.

Siku ya jumapili januari mosi mwaka 2017 kutakuwa na kilele cha tamasha la michezo kwa kuzikutanisha timu asimu maarufu watani wa jadi mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya timu ya Hawili fc dhidi ya Sido fc mchezo utakaotimua vumbi uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale

Post a Comment

 
Top