0

VIOJA mbalimbali vimetawala jana kwenye mazishi ya Denes Komba [26]mkazi wa Mateka kisiwani Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambaye alidaiwa kuwa alifariki dunia baada ya kuuawa kwa Nyoka ambaye alimhifadhi kwenye mfuko wa koti ambalo alikuwa amelivaa.

  Wakizungumza na mtandao  huu kwa masharti ya kutokutaja majina yao baadhi ya majirani waliyohudhuria mazishi hayo ambayo yanadiwa yalifanyika bila kufuata  imani  ya dini yeyote  walisema kuwa wao walipotaka kwenda kukesha kwenye msiba kabla ya mazishi walikatazwa na baadhi ya wanandugu wa marehemu kwa madai hapana msiba kama watu wanavyo dhania.

 Walisema kuwa licha ya kukataliwa kuwa hapo hapana msiba walijitahidi kuonyesha upendo wa kusubiri kutambua nini kinaendelea na ilipofika Desemba 28 majira ya saa tano asubuhi waliona gari likiwa limepakia msiba likiendeshwa kwa kasi kuelekea makaburi ya Mateka kisiwani ambapo ndipo ulipozikwa mwili huo.

 Majirani hao walisema kuwa hakuna kilichoendelea baada ya mazishi ambayo hayakusimamiwa na imani ya dini yeyote ile kama misiba mingine ilivyozoweleka kwa majirani kushirikiana pamoja na viongozi wa kidini.

 Kwa upande wake mmoja ya watu ambao walikuwa karibu na marehemu Komba ambaye naye hakutaka kutaja  jina lake alisema kuwa Denis Komba inadaiwa kuwa  Nyoka huyo alikuwa naye siku nyingi kwani hata kindi cha nyuma alikuwa anawatishia nalo wakiwa kwenye michezo uwanjani.

 “Tuliwahi kumuuliza kuwa wewe nyoka umempata wapi alisema mimi mniache sihitaji maswali kutoka kwenu huyu nyoka nimepewa ninyi hawawahusu bila kumtaja aliyempatia”alisema kijana huyo ambaye anadai walikuwa ni marafiki.

  Habari zilizopatikana mtaani hapo kuwa siku ya tukio ambayo Nyoka huyo aliuwawa na kumfanya Denis Komba kufariki Dunia kisha Nyoka huyo kuchukuliwa na Maliasili ambaye walienda kumtupa vichakani inadaiwa bibi wa marehemu alijitahidi kuwatuma watu kwenda kumchukua.

 Tukio  la kifo hicho lilitokea Desemba 26 mwaka huu majira ya saa 1.30 usiku huko katika eneo la barabara karibu na ofisi za kampuni ya simu Tanzania [TTCL]iliyopo Songea mjini jirani na Hospital ya serikali mkoa huo wakati Denis Komba na mwendesha boda boda Kasian Haule aliyekodiwa na Komba wakitokea kijiji cha Mpitimbi kilichopo Songea vijijini na kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji alidhibitisha kutokea kwa kifo hicho.

chanzo:ruvuma tv

Post a Comment

 
Top