November 4 2016 iliripotiwa kwenye Magazeti kwamba Mbunge na Mwanasheria wa CHADEMA
Tundu Lissu anatakiwa kukamatwa kwa amri ya Mahakama baada ya
kutotimiza masharti ya Mahakama kwa kuhudhuria kwenye kesi yake
inayomkabili Kisutu Dar es salaam.
Polisi kanda maalum ya Dar es salaam kupitia kwa kamishna wake Simon Sirro
imesema sababu za kwanini Tundu Lissu hajakamatwa mpaka sasa ni
kutokana na Polisi kutopokea hati yoyote kutoka Mahakamani Kisutu
inayoagiza kukamatwa kwa Tundu Lissu lakini ikiwafikia tu watafanya
hivyo.
Post a Comment