0

 Mchezaji wa timu ya Likongowele fc akimiliki mpira wakati wa mchezo dhidi ya Black stars uliopigwa novemba 4 katika uwanja wa hamlashauri ya wilaya ya Liwale.


                         Mchezaji wa timu ya Black Stars akirusha mpira 

Matokeo ya mchezo wa novemba 4 kati ya timu ya Likongowele fc dhidi Black Stars katika ligi daraja la nne inayoendelea uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,Likongowele fc waliibuka na pointi 3 muhimu baada ya kutikisa nyavu mara 3-1.


magoli ya timu ya Likongowele yalifungwa na Shafii Masii dakika ya 18,John John dakika ya 60 na goli la mwisho likifungwa na Ngauga Ngauga katika dakika ya 86.


Goli la kufutia machozo la timu ya Black Stars lilifungwa na Juma Mataka dakika ya 66.


 Mara baada ya kumalizika kwa mchezo kocha wa Black Stars,Maulidi Mpalama alizungumza na Liwale Blog alisema mchezo huo ulikuwa na matatizo kwa upande wa waamuzi wote na anatarajia kukata rufaa nae kocha wa Likongowele fc,Mahela Mahela alisema alichokifundisha ndicho walichofuata wachezaji wake na kupelekea kupata ushindi wa magoli 3-1.


Baadhi ya wadau wa mpira wakizungumza na Liwale Blog, Matata Mitambo alisema timu nyingi zinalalamikia upande wa waamuzi wa mchezo hawachezeshi vizuri hivyo ameomba uongozi wa soka hapa wilayani (LIDIFA) kuwaleta wakufunzi ili kuweza kuwafundisha ili kuweza kuibua vipaji vya vijana pia aliongeza kushauri uwanja wa halmashauri unatakiwa uboreshwe.


Nae Nassoro Nassoro aliseama ligi daraja la nne inaendelea vizuri kiasi lakini aliwatupia lawama kwa upande wa mashabiki kitendo cha  kuwakamia na kuwatishia kuwapiga waamuzi wa pembeni washika vibendera wakati wapo kwenye majukumu yao kwakuwa uwanja wa halmashauri hauna uzio hadi kumfikia mwamuzi wa pembeni na aliomba upande wa vyombo vya usalama kufanya kazi yao wakati wa mchezo kwa kuzunguka kona zote za uwanja.
Katika hatua nyingine mashabiki wa soka walalamikia wamiliki wa uwanja wa halmashauri kitendo cha kufungwa kwa  vyoo  uwanjani hapo wakisema hawatendewi haki kwani wanalipia kiingilio wakati wa mechi na wakibanwa na haja ndogo  kulazimika kujisaidia mahali popote mwa uwanja huo kitendo ambacho si cha ungwana  huku wakidai baadhi ya vyoo uwanjani hapo vimekamilika lakini wanashangaa kuona bado vimefungwa.


kijana akiwa pembezoni wa geti la uwanja wa uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale akijisaidia haja ndogo
vyoo vinavyodaiwa vimekamilika lakini vikiwa vimefungwa na hapa kari na geti ikionekana chupa yenye mkojo imetupwa chini.
Pia pembezoni mwa geti kwenye vyoo vinavyodaiwa vimekamilika lakini vimefungwa mashabiki hutumia mahali hapa kujisaidia haja ndogo.


Post a Comment

 
Top