*Maajabu yetu Waafrika tuyafanyayo kwa jina la "UTAMADUNI WETU"*
*1 Tunamjali sana mtu akirehemika kuliko akiwa hai*
*2.Tunagharamia mno kuwazika marehemu kuliko kuokoa maisha alipokuwa anaumwa.*
*3. Hatusafiri kwenda kumsalimia ndugu anayeumwa, bali twasafiri wengi kwenda kumzika.*
*4.Ni nadra sana watu kukupa heshima ungali hai, lakini watapenda sana kukupa heshima za mwisho eti ukiwa kwenye jeneza*
*5.Wewe hujawahi kupewa ua na mtu yeyote tangu uzaliwe, lakini watalundika maua mengi mno juu ya kaburi lako*
*6.Utakesha msibani kwa jirani yako kwa kuwa amefariki, ila hukuwahi kufika ndani kwake hata siku moja akiwa hai/mgonjwa.*
*7.Ukiwa hai hakuna anayetaka kujua kijiji unachotoka, ila ukifa, watajaa kwenye magari wasindikize jeneza lenye mwili wako kukiona hicho kijiji*
*NATOA USHAURI:*
*1.Tuwajali watu wakiwa HAI kwanza 2.Tubadilike kimtazamo wa Utamaduni, tuangalie maendeleo ya waliobaki HAI*
Post a Comment