NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM
BARAKA Elias (35), kijana mwenye urefu wa futi 7.4 anayesubiri kufanyiwa
matibabu ya kubadilisha nyonga yake ambayo imevunjika, hatapewa tena
rufaa ya kwenda nje ya nchi kufuata matibabu hayo.
Badala yake atafanyiwa upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) ambako anapatiwa matibabu ya kutuliza maumivu yanayomkabili hivi sasa.
Mkurugenzi wa MOI, Dk. Othuman Kiloloma alisema hayo jana alipozungumza na MTANZANIA.
Gazeti hili lilitaka kujua hatma ya matibabu ya kijana huyo ikizingatiwa awali MOI ilishindwa kumfanyia upasuaji huo kutokana na umbile lake.
Ilielezwa kwamba madaktari walishindwa kumtibu kwa sababu mashine za MOI hazikuwa zinalingana na urefu wake.
Mkurugenzi huyo alisema baada ya changamoto hiyo kujitokeza, walilazimika kuunda jopo la madaktari ambalo lilifanya tathmini ya matibabu ya kijana huyo.
“Kwa kuwa umbo lake ni kubwa ikilinganishwa na watu wengine, tulipokwama awali ilitulazimu kuunda jopo la madaktari kufanya tathmini na uamuzi wa hatma ya matibabu ya Elias.
“Jopo hilo lililokuwa likiongozwa na Daktari wetu, Lupondo, tayari limefanya tathmini na imeonekana kwamba kifaa anachohitaji kinaweza kupatikana, hivyo badala ya kumpa rufaa kwenda nje tumewasiliana na nchi tatu tupate kifaa hicho,” alisema.
Dk. Kiloloma alitaja nchi ambazo wamewasiliana nazo kupata kifaa kinachohitajika kufanikisha upasuaji huo kuwa ni Ujerumani, Marekani na India.
“Hawa wana viwanda vinavyotengeneza kifaa hicho kwa ubora, hatujajua hadi kitakapofikishwa hapa kitagharimu kiasi gani itategemeana na bei ya ununuzi.
“Na kwa sababu ya umbile lake watalazimika pia kubadilisha kidogo mfumo wa mashine zao kupata kile kitakachomtosheleza mgonjwa wetu… kwa hiyo bado hatujajua pia kitawasili lini nchini,” alisema.

Post a Comment