Serikali ya Algeria imepitisha mswada wa kubana
matumizi unaojumuisha kuongezwa kwa kodi na kusimamishwa kwa mishahara
ili kukidhi kushuka sana kwa mapato yapatikanayo kutokana na mauzo ya
gesi.
Wengi wa wabunge wa chama tawala Algeria waliuidhinisha mswada huo hapo jana huku wabunge wa upinzani wakisusia kura hiyo.
Mohamed
Djemai, mbunge wa chama tawala cha National Liberation Front, amesema
ameunga mkono mswada huo kwani hauathiri mafao ya kimsingi ya kijamii ya
Waalgeria, licha ya matatizo ya kiuchumi.
Wanaoupinga mswada
huo, wakiwemo walimu na wahudumu wa afya nchini humo, wamepanga kufanya
maandamano kuanzia tarehe 27 hadi 29 mwezi huu.
Mabadiliko katika bajeti yatapelekea kuanzishwa kwa kodi mpya na kuongezwa kwa bei za tumbaku, pombe na mafuta.
Wakosoaji
wa mswada huo wanaishutumu serikali na matajiri kwa kujilimbikizia mali
nyingi, ilhali wananchi wa kawaida wakitaabika na mfumko wa bei.
Post a Comment