0
“Katika wasifu ametajwa mke wa marehemu mmoja lakini mimi nawafahamu wake wa marehemu wengi sana. Na katika tabia zetu za kiafrika hilo suala la wake wengi ni kawaida tu. Hata vitabu vitakatifu vinasema Mfalme  Suleiman alikuwa na wake zaidi ya elfu moja.
“Nilikuwa naongea pale na Mheshimiwa Kikwete nikasema na sisi tungefurahi sana kama tungekuwa na wake wengi kama hawa,” amesema na kusababisha vicheko na miguno kutoka kwa waombolezaji.
Rais Magufuli ameeleza kuwa, historia ya Masaburi haiwezi kufutika katika Jiji la Dar es Salaam ushahidi wa hili ni watu wengi waliojitokeza katika msiba wake.

“Tunazungumza hapa kuwa watoto wa marehemu ni 20 lakini wanaweza kuwa hata zaidi ya 20.
“Niwaombe sana nyie watoto msifarakane, mshikamane na mtoto wa kwanza akawe kiongozi wa familia, palipo na umoja Mungu atawatangulia, sisi sote tu njia moja na kila mmoja ataionja mauti na si mimi, Kikwete wala Lowassa atakeyekwepa mauti,” amesisitiza.

Baada ya mwili huo kuagwa Karimjee, msafara wa waombolezaji umeelekea eneo la Chanika kwa ajili ya mazishi.
Viongozi mbalimbali walijitokeza kuuaga mwili huo pamoja na wananchi mbali na Rais Magufuli ni Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu; Rais Mstaafu Kikwete; Spika Mstaafu, Anne Makinda na Gharib Bilal, Makamu Mstaafu wa rais.

Post a Comment

 
Top