Kufuatia
hatua ya Serikali kununua hisa zote za Bharti Airtel ambaye alikuwa
mbia mwenza wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na hivyo Serikali
kumiliki hisa za Kampuni hiyo kwa asilimia 100, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Waziri Waziri
Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Waziri
Waziri Kindamba ameteuliwa kushika nafasi hiyo kuanzia leo September 23
2016. Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt.
Kamugisha Kazaura atapangiwa kazi nyingine.
Post a Comment