0

Ikufikie hii mtu wangu wa nguvu, Nafahamu bado haujasahau matukio yaliyoripotiwa kutokea kwenye nchi nyingi duniani kuhusu mauaji ya raia wakiwa kwenye mikono ya polisi. Leo imenifikia ripoti hii ikionesha idadi ya watu waliouawa na askari police kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
Ripoti hii ni kwa mujibu wa gazeti la Washington Post la nchini Marekani wametoa idadi ya watu walifariki kutokana na kupigwa risasi iwe ni kwa makusudi au bahati mbaya wakiwa chini ya ulinzi wa polisi, Washington Post wanasema jumla ya watu 990 wamekufa wakiwa chini ya polisi.
Wakati kwa Ujerumani, imeonesha watu 9 pekee ndio waliouawa mwaka jana, taarifa hii ni kwa mujibu wa ripoti ya siku ya jana September 22, 2016, iliyotolewa na kampuni ya uchapishaji ya Funke Mediengruppe kutoka Ujerumani, iliyofanyiwa utafiti na chuo cha polisi cha Ujerumani.
Ripoti hiyo pia imeonesha idadi ya watu waliopo nchini Marekani ni mara nne zaidi ya waliopo Ujerumani. Mwaka huu pekee, watu wameuawa na askari polisi wa Marekani, kwa mujibu wa Washington Post. Na kuanzia January 5, mwaka 2016, watu 13 wameuawa na polisi nchini Marekani ikiwa ni zaidi ya watu waliokufa nchini Ujerumani kwa mwaka 2015.

Post a Comment

 
Top