Mahakama
ya katiba nchini Gabon imethibitisha kuwa Ali Bongo ndiye mshindi wa
uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 27 nchini humo.
Rais Bongo amepata 50,66% na mpinzani wake, mwenyekiti wa zamani wa Muungano wa Afrika Jean Ping 47,24%.
Matokeo ya awali yalionyesha ushindi wa Bongo kwa tofauti ndogo ya kura takriban 6000.
Kwa
mujibu wa matokeo ya mwisho rasmi yaliotolewa na mahakama ya katiba
Bongo alishinda na kura zaidi kutokana na kutobatilisha kura zilizopigwa
katika ngome ya kiongozi huyo Haut-Ogoue.
Hatahivyo
kura katika vitu 21 mjini Libreville zimefutiliwa mbali kutokana na
ombi la upande wa kampeni ya rais. Na ndio sababu kiongozi huyo amepata
asilimia kubwa zaidi katika matokeo ya mwisho.
Upinzani uliwasilisha malalamiko kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi na
kuiomba mahakama iamrishe kuhesabiwa upya kura hizo, katika eneo hilo
la Haut-Ogoue, magharibi mwa Gabon ambapo rais Bongo ana wafuasi wengi.
Kumekuwa na wasiwasi katika mji mkuu Libreville kwamba huenda ghasia zikazuka baada ya mahakama ya katiba kutoa uamuzi wake.
Baadhi ya wakaazi walionekana kununua vyakula na kuweka akiba nyumbani.
Raia mmoja ameiambia BBC: " Nadhani kuna wasiwasi, watu wanataka kuwa
salama, wanataka kununua vitu na kusubiria matokeo kwa makini nyumbani,
iwao kila kitu kitakwenda sawa itakuwa vizuri"
Maduka mengi yameamua kufunga biashara kukwepa uporaji.
Post a Comment