Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani litaanza upimaji na matibabu kwa madereva nchini
Hatua hiyo inakuja baada ya kupokea vifaa mbalimbali ikiwemo stika elfu moja, fulana elfu moja, kofia mia tano pamoja na kliniki ya upimaji magonjwa, kutoka kampuni ya bia nchini (TBL) kama sehemu ya kusaidia kampeni ya Wiki ya Usalama Barabarani.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Mohammed Mpinga amepokea vifaa hivyo kutoka kwa Afisa Uhusiano wa TBL Bi. Amanda Walter na kwamba sehemu ya vifaa hivyo vitatumika kupima afya kwa ajili ya kubaini magonjwa mbalimbali yanayowasumbua madereva na ambayo iwapo yatatibiwa yatasaidia kupunguza wimbi la ajali za barabarani zinazotokea maeneo mbalimbali nchini.
Huduma ya upimaji itatolewa na Zahanati Mwendo (Mobile Dispensary) inayomilikiwa na Bi. Rosemary Mwakitwange ambaye yeye na daktari wa zahanati hiyo wameyataja magonjwa yatakayopimwa kuwa ni UKIMWI, macho, moyo na aina nyingine za magonjwa ambayo huwashambulia madereva mara kwa mara.

Post a Comment