0


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kila msaada wanaopata kwa ajili waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera utapelekwa Bukoba na kugaWiwa kwa walengwa huku akiahidi kuwa serikali itahakikisha waathirika wote wanafikiwa na misaada hiyo.

Akiongea leo Jijini Dar es Salaam baada ya kupokea msaada wa zaidi ya shilingi milioni 40 zilizotolewa na makampuni mawili tofauti, Mhe. Majaliwa amesema misaada yote ya vyakula na vifaa vya ujenzi itapelekwa yote Bukoba na kugaiwa kwa walengwa.

Akizungumzia shule za mbili za Ihungo na Nyakato ambazo majengo yake yameharibika kutokana na tetemeko la ardhi Kagera na kupelekea shule hizo kufungwa Mhe. Majaliwa amesema wamepata wafadhili ambao wamejitokeza kuzijenga.

Post a Comment

 
Top