Kijana mwenye umri
wa miaka 19 mkazi wa jimbo la kaskazin magharibi mwa Nigeria la Bauchi
anasema kuwa macho yake yalitolewa na watu waliotaka kuyatumia kwa ajili
ya sababu za ushirikina.
Viungo vya mwili wa binadamu ambavyo
hutumiwa katika imani za uchawi ama kwa ajili ya mazingaombwe hutolea
kutoka kwa watoto nchini Nigeria, na mara nyingi watu wazima huwa
hawaathiriwi.
Hussain Emmanuel, ambaye kwa sasa anatibiwa katika
hospitali ya mji wa Bauchi, anasema shabulio lililomuacha bila uwezo
wa kuona tena, lilitokea wiki mbili zilizopita katika kijiji kilichoko
eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi la Tafawa Balewa.
Anasema alirubuniwa na watu wawili katika kijij cha Marti kilichopo karibu na mto waliomshawishi aende kuogelea .
Bw
Emmanuel, ambaye hufanya kazi yake ya kibinafsi kama fundi wa magari,
anasema alikuwa pamoja na watu hao wawili kwasababu mmoja wao alimuahidi
kumpa kazi kusini mwa Nigeria.
Lakini walipokwenda mtoni
walimshabulia, wakataka kumnyongana na mnyororona shingoni na baadae
wakaamua kumgonga kiasi cha kupoteza fahamu.
Alipoamka, hakuweza
kuona , ndipo alipopiga mayowe hadi alipookolewa na wapita njia ambao
walibaini kuwa macho yake mawili yalikuwa yameondolea.
Polisi
wanasema wanachunguza kisa hicho, na hawakutoa kauli yoyote kuhusiana na
sababu ya washukiwa hao kutekeleza kitendo hicho.
Washukiwa wote wawili bado hawajakamatwa.
Post a Comment