Nchi za Marekani na
Uchina ambazo kwa pamoja huzalisha gesi chafu ya kaboni duniani kwa
40% - sasa zimeidhinisha mkataba wa Paris wa mabadiliko hali ya hewa
duniani.
Baada ya kuwasili napamoja na viongozi wengine wa mataifa
ya G20 kwa mkutano katika jiji la Hangzhou, rais wa Marekani Barack
Obama amesema: " Historia itahukumu juhudi za leo kama za la muhimu na
mafanikio."
Kupunguzwa kwa gesi aina ya CO2 ndilo lengo linalotegemewa katika mabadiliko ya hali ya hewa.
Hatua
kubwa kuelekea utekelezwaji wa makubaliano haya ilifikiwa mwezi
Disemba, ambapo mataifa hayo yalikubaliana kupunguza gesi chafu kwa
kiwango cha kuwezesha kupanda kwa joto la dunia kufikia chini ya nyuzi
joto 2.
Mapema Jumamosi wajumbe wa kamati ya bunge la taifa la
kongresi la watu wa Uchina- China's National People's Congress
waliidhinisha "pendekezo la kuchunguza upya na kuidhinisha mapatano ya
Paris " Jumamosi asubuhi katika kilele cha wiki nzima cha vikao vya
bunge.
Mkataba wa Paris ni mapatano ya kwanza kuwahi kuzingatiwa
zaidi miongoni mwa makubaliano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa
duniani.
Utekelezwaji wake utakubalika rasmi kisheria baada yakuidhinishwa na nchi 55 zinazozalisha 55% ya hewa ya Kaboni duniani.
Post a Comment