0

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Alain Nyamitwe, amekiri umuhimu wa mazungumzo baina ya wadau Burundi endapo tu yataheshimu katiba ya nchi hiyo.

Bwana Alain amesema hayo wakati wa hotuba yake kwenye kikao cha 71 cha Baraza Kuu ambapo amesema wananchi wametoa wito wa mabadiliko muhimu yanayohitajika kuleta amani, katika ripoti ya iliyotolewa na tume ya uchunguzi, wito ambao serikali ya Burundi umeyasikia na unayazingatia.

Pia amesisitiza kuwa serikali yake inahakikisha usalama wa raia wote na kuimarisha haki za binadamu, bila kujali kabila, huku akisisitiza kuwa ni lazima tathmini zozote zinazohusu haki za binadamu nchini Burundi zitekelezwe kwa tahadhari kwani Uvumi, habari za uongo, mitandao ya kijamii, haya yote yanatumika kuipa Burundi taswira mbaya.

Halikadhalika, amesema nchi yake itawasilisha ripoti kamili mbele ya kamati dhidi ya utesaji Geneva, inayokanusha madai yoyote kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo. Pia amesema anaamini kamwe hakutakuwa na mauaji ya kimbari nchini Burundi na wananchi wake wanapinga vikali jinamizi hilo.

Post a Comment

 
Top