0


Nyumba na maduka manne yameungua moto huku baadhi ya vyumba na vitu vyote vilivyomo ndani vimeteketea,moto huo umetokea jana katika mtaa wa Mfaranyaki manispaa ya songea mkoani Ruvuma chanzo cha moto huo imeelezwa kuwa ni mpangaji mmoja aliacha jiko la gesi likiwa linawaka naye akiwa nje ya nyumba hiyo kwa kitambo kirefu.

Mwenyekiti wa mtaa huo Lufina Luoga amemtaja mmiliki wa nyumba hiyo kuwa ni Eddu Hunja na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni jiko la gesi lililoachwa likiwaka kwa muda mrefu kulipuka na kusababiusha shoti ya umeme kabla ya kikosi cha zimamoto na uokoaji hakijafika wananchi walijitokeza kwa wingi kusaidia kuokoa mali za duka na vyumba vilivyokuwa wazi ambapo sehemu kubwa ya mali za duka ziliokolewa.

Mmiliki wa nyumba hiyo,Eddu Hunja amesema kuwa alipigiwa simu na mpangaji wake akijulishwa juu ya tukio hilo alipofika eneo la nyumba yake aliwakuta wasamaria wema wakiokoa vifaa vya ndani na gari la zimamoto lilikuwa limeshawasili na kuanza kazi ya uokoaji na kuzima moto.

Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoani Ruvuma Frolence Daniel amewataka wananchi kukariri na kuitunza namba ya ya dharula ya jeshi hilo 114 pindi ajali ya moto inaptokea amesema kuna mazoea mabaya baadhi ya wananchi hawaoigi simu badala yake wanakwenda kituoni kutoa taarifa wakati moto unaendelea kuwa jambo ambalo linasababisha jeshi kulaumiwa kuwa wanachelewa kufika eneo la tukio.

Post a Comment

 
Top