August
30 2016 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa amefungua mafunzo ya wakufunzi wa marubani katika chuo cha Taifa
cha usafirishaji (NIT).
Waziri
Mbarawa ametumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kwamba Serikali
haikukurupuka katika kufanya maamuzi ya aina ya ndege za kununua badala
yake imezingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri wa ndani
na kuboresha usafiri wa anga kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Amefafanua
zaidi kuwa Serikali iliamua kununua ndege mbili za abiria aina ya
Bombadier Q400 kutoka nchini Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya
usafiri wa anga kwa safari za ndani ya nchi na mazingira halisi ya
viwanja vya ndege vilivyopo nchini.
>>>‘Serikali
imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier Q400 kutokana na hali
halisi ya Viwanja vya ndege nchini kuwa vya Changarawe na lami kwa
baadhi, huku lengo ni kutoa huduma za usafiri wa ndani’ ;-Waziri Mbarawa.
Aidha
Waziri Mbarawa aliwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni
kuhudumia wananchi hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu ndege hizo kwani
zimezingatia mambo mbalimbali ikiwemo suala la usalama na ufanisi
katika uendeshaji wake.
Aliongeza
kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutua katika viwanja vingi hapa nchini
kwani zinaweza kutua katika viwanja vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo
ndio vingi nchini tofauti na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja
vyenye urefu zaidi ya kilomita mbili.
Prof.
Mbarawa alibainisha sababu nyingine kuwa ni aliongeza uwezo mdogo wa
ndege hizo katika kutumia mafuta ukilinganisha na aina zingine ambapo
kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza zitakuwa zikitumia Tani
1.7 za mafuta tofauti na aina nyingine zinazotumia hadi Tani 2.8 kwa
safari moja.
Waziri
Mbarawa pia alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa ndege
hizo zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na sifa na kubainisha
kuwa suala hilo siyo la kweli kwani kampuni hiyo imefanya biashara na
nchini nyingi ikiwemo Ethiopia yenye ndege t19 aina ya Bombadier Q400
zilizotengezwa na Kampuni hiyo.
Mpaka sasa
tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo kwa
asilimia 40 ambapo ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchini September 19
mwaka huu ambapo zitaanza safari ya kutoka nchini Canada tarehe 15
septemba mwaka huu kupitia nchini Uingereza.
Post a Comment