0

 Mwanamume mwenye asili ya kihindi alitozwa faini ya Ksh 10milioni na mahakama kwa kukosa kumpa mapenzi mkewe

Mwanamume kutoka Mombasa ametozwa faini ya KSh 10 milioni kwa kukosa kushiriki mapenzi na mkewe kwa miaka 18.

Patel alimuoa Sonia chini ya tamaduni za Kihindi kabla yao kuhamia Mombasa.

Hata hivyo, mke huyo adai Patel hakumuambia kuhusu tatizo lake la nguvu za kiume kabla yao kufunga ndoa.

Vile vile, alidai kugeuzwa mjakazi wa nyumbani walipowasili Mombasa, ambako walikuwa wakiishi na familia ya Patel eneo la Nyali.

Sonia aliamua kwenda mahakamani kuifuta talaka ambayo Patel alimpa 2009 na kesi hiyo kufika mbele ya Jaji Maureen Odero.

Mwanadada huyo asema licha ya kukosa mapenzi, ndoa yao ilikuwa ya furaha na utulivu, ijapokuwa mambo yalibadilika baada ya babake Patel kuaga dunia.

Mwanamke huyo ameeleza kuwa Patel aligeuka kuwa katili, mpenda vita na dhuluma; akawa anamshinikiza Sonia arejee kwao India.

Sonia aliiambia korti kuwa hawakuwahi kushiriki mapenzi katika muda wote wa miaka 18 walipokuwa katika ndoa.

Mke huyo aliamua kustahimili ndoa kavu bila mapenzi kwa sababu talaka ni mwiko katika jamii ya Kihindi.

Kwa upande wake, Patel alisema mkewe alikuwa amemtangaza na kumkejeli akisema kuwa ni ‘bwege’ kitandani, jambo lililomletea aibu kubwa.

Jaji Odero aliamua Patel kumpa Sonia KSh10 milioni kwa wakati mmoja ama KSh4.25 milioni kwa awamu katika siku 60.

“Ulaghai wa mwanamume huyu ni ukatili mkubwa. Uliyafanya maisha ya mkewe kuwa makavu bila mapenzi –jambo ambalo ni uchu wa kila mwanamke aliye katika ndoa,” akasema.

Jaji Odero alisema Sonia alihadaiwa kuingia katika ndoa kwa misingi ya uongo, akahamishwa hadi taifa geni na kugeuzwa mjakazi wa nyumbani.

Post a Comment

 
Top