SEHEMU YA SABA
Yale
maneno hayakuwa msumali tu kwangu na kumbe yalikuwa ya kichoma choma vibaya
mno, namna nilivyokuwa nikiyaongea nilishangaa mama machozi ya kimtoka. Nilisita
kidogo kumalizia yale maneno ambayo yalikuwa yakinitoka hata sikujua kama
niliyapangilia ama la maana niliona yanakuja kwenye kinywa changu na kuyatamka.
Nilikuwa
kimya kidogo, nikiwa na mtazama mama kwa makini, nikitaka kusema jambo tena,
ila kabla sijasema. Mama aliianza kuongea, maneno ambayo hakika sitakuja
kuyasahau kabisa, najua mama yangu alikuwa akijua nini alichukuwa anakisema.
"Criss
mwanangu we ni tegemeo langu sana kwa sasa we ndio
maisha yangu hakika mwanangu naomba uwe mbali sana na wanawake na kama
utashindwa baba, kwa sababu najua sasa umekuwa mkubwa kwa sasa, basi baba yangu
naomba ufanye uchaguzi sahihi. Yote kwajili ya maisha yako mwanangu nakupenda
sana sipendi nikiona unapata tabu kama kaka yako Eddy.
Sijui
nini kilimtokea hakuwa mtu, wanawake tulimlea vizuri sana mimi na marehemu Baba
yako. katika misingi mizuri ya dini kama tulivyokulea wewe, lakini baba kupenda
hakuna mwenyewe upendo wa kimapenzi unakujaga pasipo mwenyewe kutegemea.”,
Alisita kidogo mama huku akinitazama, nikiwa kimya tu. Macho yangu yaliweza
kubainia maneno yake yalikuwa yana maana kubwa sana katika maisha yangu.
Mama
hakuishia hapo aliendelea baada ya kunitazama kwa muda kidogo. “Siwezi kumlaumu
kwa jambo hilo na jua Bibilia inasema vyema Mungu alituleta dunia kwa jili ya
mapenzi yake, nasi hatuna budi tupendane, tuzaliane ilituijaze dunia. Ila
mwanangu chunga mwanamke utayekuja kumpenda hakikisha ni wa namna tofauti na
mwenye upendo wa dhati na wewe”. Mama akuishia hapo, mara aliniuliza swali ni
nikabaki nakodoa macho huku
nikiliona nilikuwa katika mtihani mzito
sana katika maisha yangu.
Sikuwa
na la kujibu maana sikuwa na jua juu ya jambo lile, halikuwa swali lingine bali
lilikuwa likiwa likimuhusu kaka Eddy. Nilitulia ndugu msikilizaji nikabaki
kimya, kabisa kimya ambacho kilifukuzwa na maneno ya mama, huku akiyatalawa
mazungumzo kwa kiasi kwamba nilibaki kuwa msikilizaji.
“Sikiliza mwanangu Criss, katika maisha ya kaka
yako Eddy yana siri nzito juu ya ndani yake, lakini kwa sasa sidhani kwa wakati
wake wa wewe kuijua siri hiyo, wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.
lakini kwa sasa hivi nitakuwa na kubebesha mzigo sana na chuki zisiokuwa na
sababu cha msingi mwanangu”.
Mama
aliongea kwa hisia mno sana, maneno yale, niliyapokea katika mtazamo ulijaaa udadisi
kama kawaida yangu, sikuiacha hiyo tabia.
Juu ya neno siri tena si siri ya kawaida ni nzito kidogo jambo hilo lilinza kuleta
walakini kidogo ndani ya kichwa changu. Jambo gani lililojificha juu ya kaka
Eddy?, sasa ukawa mtihani ndani ya kichwa changu huku nikihitaji majibu yenye
tija juu ya jambo lile, likionenakana muhimu sana katika maisha yangu. Maana
mama alishawaniambia lazima angeweza kuniambia lakini si kwa mapema kama shauku
yangu ya kutaka kufahamu ilivyokuwa ikiniongoza.
____________
Jina
la Irene likarudi kichwani kwangu, ndugu msikilizaji, ni huyo Irene ambaye
niliweza kufahamu kwa uchache yalikuwa yakimuhusu japo kuwa sura yake
ilishapotea siku nyingi kichwani mwangu.
Niliitaji kumfahamu zaidi Irene, nilijiapiza kufatiria mwanzo mwisho kujua
kilichopo nyuma ya lile.
Wakati huo nilikuwa kimya nikiendelea kumsikiliza mama alichokuwa anasema ndani
ya kinywa chake, ilikuwa si kawaida kabisa kumuona mama yupo kwenye hali ile.
Kiukweli tangia kipindi chote cha likizo yangu, siku hiyo ilikuwa yupo tofauti
sana hata hali ya uchangamfu ilimpotea. Jambo lile ilionekana lilimuumiza sana
ndani ya moyo wake. Nilimjua mama si mtu wakupenda kuona mimi napata tabu, eti
kisa kitu fulani.
Furaha
yangu ndio furaha yake, huzuni yangu ndio huzuni yake.
"Nadhani
umenielewa usifikiri chochote mwanangu Criss nipo pamoja na wewe sahau chochote
kuhusu haya unajua vyema umebakisha siku chache ufanye mtihani wako wa kumaliza
elimu ya kidato cha sita hivyo jaribu kutulia kupunguza mawazo yasio kuwa ya
msingi yatakuharibia mambo yako mwanangu umenielewa?”. Aliniuliza mama nami
nikamjibua kwa kutikisa kichwa kuonesha nimeelewa kile alichokuwa anazungumza
katika yale mazungumzo.
_____
Wakati
huo muda ulishaenda sana, na hata jua lilianza kuchoma choma na kuongeza joto
mwili, kuikaribisha mchana wa siku hiyo.
Ni nyakati hizo ambazo mama aliniaga, na kuniachia pesa kidogo ya
kufanya matumizi na yeye akilielekea kwenye mikutano yao ya kinamama.
Nirejea
chumbani kwangu punde mama aliponiacha, njaa haikuwa ikisumbua tumbo langu,
ijapokuwa nilikuwa sijapata kuingiza chochote ndani yake. Nilirudi ndani na kujitupa kitandani kwa mara
nyingine.
Nikiwa
kitandani kwangu nilitulia kimya ni kitafakari yale mama aliyoniambia muda
mchache kabla ajatoweka kwenye macho yangu.
Nikiwa nayafikiria yale mazungumzo mara nikakumbuka lile jambo la siri.
Nikajiuliza mara mbili ni siri gani hiyo?. Fikra zangu zikaonesha kunisaliti,
kabla ya kuleta tumaini, tumaini ambalo pekee fikra zangu zikinikumbusha naweza
kulipata ndani ya kijitabu alichokiandika
mwenyewe kaka Eddy pasipo kulewa kilikuwa na maana gani katika maisha
yangu.
Macho
yangu yakaanza kukitafuta wapi nilipokuwa nimekitupa, baada ya kumbukumbu
zangu, kupotea mahala nilipokuwa nimekiweka. Maana nilipozoea kukiweka
hakikuoneka. Mwanzoni niliona haitakuwa ngumu kukipata lakini kadri muda
ulivyokuwa unaenda ndio ugumu ulizidi kuongezeka. Nilichanganyikiwa kwa kweli
ndugu msikilizaji.
Post a Comment