0

Katika maisha yetu ya kila siku neno fursa si geni sana masikioni mwetu.Neno hili watu wengi hulichukulia kama la kawaida sana lakini kiukweli kama utaweza kujua maana yake na kufanyia kazi lazima utaona mabadiliko makubwa katika maisha yako.Fursa nyingi hapa duniani zinakuwa haziko wazi au kwa maneno mengine zinakuwa zimejificha sana.Leo hii nataka nikushirikishe njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuona fursa mbalimbali katika eneo lako.

1. Tambua fursa ikoje
Ili uweze kuona fursa katika maisha lazima ujue kwanza fursa ni nini na inafananaje.Kwa mfano unaweza ukawa unatafuta kitu fulani lakini kwenye akili yako lazima ujenge picha ya kile kitu unachokitaka.Kwa kufanya hivi inakuwa rahisi kwa mtu kujua ni nini hasa anakitaka na atumie mbinu gani na muda gani ili aweze kufanikisha.

2. Otesha mbegu nyingi
Kuna msemo usemao usiweke mayai yote kwenye kapu moja.Kama unataka kuwa na fursa nyingi ,anza kufanya vitu vidogovidogo vingi na angalia ni kipi kinakuwa kikubwa.Kama kila kitu kitakuwa na mpango mmoja na hamna mipango mingine B,C,D au E basi utakuwa hatarini sana na pengine mpango A unaweza usifanikiwe.


3. Uwe na vigezo vinavyoeleweka 
Kwa vile fursa ziko kila mahali kama unazitafuta unapaswa kuwa na vigezo zipi nichukue na zipi niache.Jiulize maswali kama;

  • Itanifikisha karibu au mbali na malengo yangu?
  • Itanipa faida?
  • Gharama gani zitahusika?
  • Itafungua milango kwa mambo makubwa au itanipoteza? 
  • Kama itafungua milango je nilikuwa nimejopanga kwa hilo? 
  • Je nikikataa hii fursa nitafunga fursa nyingine mbeleni? 


4. Usidharau fursa ndogondogo 
Watu wengi waliofanikiwa hapa duniani walianza kufanyia kazi fursa ndogondogo zilizohitokeza machoni mwao.Kwa kuanza na fursa ndogo inakifanya upate akili ya kupambana na kuona fursa kubwa.Unaweza ukawa na fursa ndogondogo tatu kwa wakati mmoja lakini mojawapo ndo ikakufaidisha na zile nyingine zikawa zimekuongezea maarifa ya kupambana.

5. Kuwa tayari
Ili uweze kuona fursa na kuinyakua lazima uwe na utayari wa kuipokea pindi inapojitokeza.Ebu fikiria kwa kina fursa kubwa imejitokeza;je utatumia muda wa kazini?utaweza kujikimu kiuchumi?majukumu gani mtu mwingine anaweza kuyafanya kwa muda mfupi-akuangalizie watoto,aangalie nyumba yako?.Kama hivi vinakufanya uchanganyikiwe,utawezaje kunyakua fursa ikijitokeza?

Post a Comment

 
Top