Kikosi cha Mashetani wekundu
Manchester united kimeenda China katika kujiandaa na msimu mpya.Wakiwa
huko China, United watacheza mechi mbili ya kwanza watacheza na klabu ya
Borussia Dortmund mjini Shanghai, siku ya ijumaa na kisha jumatatu
watacheza na Manchester Man City,jijini Beijing.
Jumla ya
wachezaji 25 ndio wako kwenye msafara wa timu hiyo wakiwamo nyota wapya
Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan pamoja na Chipukizi tisa toka chuo cha
soka cha Man United, huku wachezaji wengine walioshiriki michuano ya
ulaya wakiachwa kuendelea kupumzika.Man United wanakwenda katika ziara hiyo wakiwa chini ya mkufunzi Jose Mourhino mwenye kibarua cha kurudisha thamani ya timu hiyo .
Post a Comment