Watumishi wengi hujutia mshahara wao kwa kukosa mambo 10 muhimu yafuatayo
1. Epuka kugeuza mshahara wako kuwa
mali ya ukoo. Kamwe mshahara wako siyo mali ya ukoo. Siku utakapoacha kuufanya
mshahara wako mali ya ukoo ndipo siku mshahara huo utakuwa mkubwa! Hapo ndipo
mshahara utatosha.
2. Siku utakapokuwa na vyanzo vya
mapato zaidi ya mshahara wako ndipo mshahara wako utakapotosha mahitaji yako ya
kila mwezi.
3. Usiombe mwajiri wako akulipe
overtime allowance, mwombe akupe muda wa kufanya kazi zako za ziada(perform
your own overtime duties)
4. Epuka kuwasambazia pesa za mshahara wako
watu wa ukoo wako ili uwaokoe na hali ngumu ya ukosefu wa fedha waliyonayo.
Badala yake Wasaidie kuona fursa za kuwapatia Pesa!
5. Usiombe mwajiri wako akuongezee
mshahara bali omba Mungu akuwezeshe Kupata kipato endelevu nje ya mshahara
wako.
6. Mtu anayeishi kwa kutegemea
mshahara wake tu ni sawa na mtu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga na
mafuriko yalipokuja anguko la nyumba hiyo lilikuwa na mshindo mkubwa sana.
7. Mto Kagera au Maragalasi haijawahi kukauka
maji yake. Kwa nini? Ni kwa sababu inapokea maji yake kutoka kwenye vyanzo
vingi vya maji au vijito vingi! Mtu mwenye vyanzo vingi vya mapato zaidi ya
mshahara atafanishwa na mto Kagera au Maragalasi isiyokauka maji yake.
8. Usisubiri kustaafu kazi ndipo ulipwe
mamilioni ya pesa za kiinua mgongo bali tafuta kumiliki vyanzo sahihi vya pesa,
na ndipo malipo ya kiinua mgongo utalipwa kila wiki mamilioni ya pesa.
9. Watu wenye busara hutafuta vyanzo vya pesa
vinavyoweza kuwalipa mshahara au pensheni ya Tshs 150 milioni kwa mwezi badala
ya kusubiri kulipwa kiinua mgongo cha Shs 150milioni baada ya kufanya kazi kwa
miaka 30 au zaidi.
10. Waajiriwa wenye hekima na busara hutumia
mishahara yao kutengeneza au kutandaza mabomba ya fedha au mtandao wa fedha
endelevu ili hata kama hawatakuwepo tena duniani watoto wao na watoto wa watoto
wao waendelee kupata mshahara kila mwezi!
Post a Comment