Siku kadhaa baada ya kuanza kwa
kambi ya mazoezi kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya wa ligi nchini
Tanzania, tayari imethibitishwa kuwa kikosi cha Mbeya City fc
kitasafiri mpaka mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu
dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri julai 30.
Kwa
mujibu wa kiongozi wa Kanisa la Faith Baptist, Mch Jerry Wyatt ambaye
ndiye mwandaaji na msimamizi mkuu wa mchezo huo,amesema maandalizi yote
ya mechi hiyo ya kirafiki itakayoambatana na tamasha kubwa la mahubiri
ya neno la Mungu tayari yamekamilika ikiwa ni pamoja na timu zote
kuthibitisha kuhudhuria.Maandalizi yote yamekamilika, timu zote zimethibitisha kushiriki katika mchezo huo ambao utaambana na mahubiri ya neno la Mungu kwenye uwanja wa Jamhuri, naomba watu wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia mchezo mzuri wa kirafiki kutoka kwa timu hizi mbili pia kupata mahubiri mazuri ya neno la Mungu hakutakuwa na kiingilio chochote kwa watakaofika kwenye uwanja wa Jamhuri .
Hii ni mara ya pili kwa Mtibwa na City kucheza mchezo wa kirafiki ulioandaliwa na Kanisa hilo awali ikiwa ni msimu uliopia ambapo timu hiyo kutoka Manungu iliibuka na ushindai wa bao 1-0 lililofungwa kipindi cha pili na Mohamed Ibrahim
City inatarajia kuondoka Mbeya Julai 28 tayari kwa mchezo huo uliopangwa kupigwa siku jumamosi ya mwisho wa mwezi huo
Post a Comment