0


Heka heka za vilabu mbalimbali barani ulaya kuimarisha vikosi vyao zimendelea kwa kusajili nyota wapya watakaozichezea timu hizo.
Klabu ya Norwich City imekamilisha usajili golikipa Michael McGovern raia wa Ireland ya kaskazini akitokea timu ya Hamilton ya Scotland kwa mkataba wa mitatu.
Nayo timu ya Burnley imewasajili winga Johann Berg Gudmundsson na golikipa Nick Pope kutoka Charlton Athletic. Wote wawili wamesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitatu huku dau la usajili likiwa halikuwekwa wazi.
Beki wa Wales Jazz Richards amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Cardiff City akitokea Fulham.

Post a Comment

 
Top