SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema katika kipindi cha miezi
mitatu imevuka malengo ya ukusanyaji wa mapato ambapo imekusanya Sh
bilioni 117.04 sawa na asilimia 99.5 ya malengo yaliyowekwa ya kukusanya
Sh bilioni 117.66.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akisema wamevuka malengo yaliyowekwa na kuifanya serikali kumudu kutekeleza na kusimamia majukumu yake kikamilifu ikiwemo kutoa huduma za jamii za afya na elimu.
Dk Mohamed alisema makusanyo ya Juni yamevuka malengo na kuvunja rekodi ambapo kabla ya hapo makusanyo ya kodi yalikuwa yamefikia Sh bilioni 82.45. Alisema kwamba mapato yamekuwa kwa asilimia 42.7 kutoka Sh bilioni 82.45 hadi kufikia Sh bilioni 117.66.
Alisema ongezeko kubwa limeripotiwa katika Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ambayo imekusanya Sh bilioni 36.04 hadi kufikia Sh bilioni 56.72 wakati Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Sh bilioni 37.1 hadi kufikia Sh bilioni 49.8.
Alisema kutokana na serikali kumudu kukusanya mapato yake vizuri katika sekta zote, imefanikiwa kulipa mishahara kwa wakati kwa watumishi wote wa serikali na taasisi zake ikiwemo mashirika ya umma.
Aidha, alisema serikali imetoa kwa mwezi Sh milioni 100 kwa ajili ya huduma za kila mwezi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja pamoja na kutoa jumla ya Sh milioni 600 kwa ajili ya kununua dawa kwa wagonjwa katika hospitali hiyo kuu.
Alikanusha kuwa serikali haijakopa fedha kwa ajili ya kulipa mishahara na huduma nyingine kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali. Naye Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Abdi Khamis amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kudai risiti wakati wanapofanya manunuzi ili kuepuka upotevu wa fedha za serikali.

Post a Comment