Waziri
mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu baada ya
kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano
wa Ulaya. Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini
kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.
Cameron
amesema kuwa kauli ya wengi lazima isikilizwe japo hafahamu kwanini
Waingereza walifanya uamuzi kama huo wakati taifa hilo lilikuwa lina
ufanisi mkubwa sana ndani ya EU.
Raia
wa Uingereza wamepiga kura ya kumaliza uanachama wa Uingereza ndani ya
EU uliodumu kwa miaka 43. Watu wanaoishi katika miji ya London na
Scotland ndio waliopiga kura kwa wingi kusalia ndani ya muungano huo.
Wadadisi
wa maswala ya kisiasa wanahofu athari za kujiondoa kwa Uingereza kwenye
muungano huo utabainika katika masoko ya hisa huku kukitarajiwa athari
kubwa kiuchumi, kisiasa ndani na nje ya bara la Ulaya.
Kura 17,410,742 zilitaka Uingereza iondoke na kura 16,141,241 walitaka Uingereza isalie
Post a Comment