Ikiwa juzi Waziri wa Fedha, Dkt Philip Mpango
kutangaza serikali kuitengea sekta ya sanaa, ubunifu, utamaduni na
michezo shilingi bilioni tatu, baadhi ya wasanii wameipongeza hatua hiyo
ya serikali ikiwa ndiyo mwanzo huku wengine wakiitaka bajeti hiyo iwe
ya vitendo na siyo maneno.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti tofauti na gazeti la Mtanzania wasanii wa muziki na
wadau pia akiwemo Mkubwa Fella alisema kuwa ni mara ya kwanza kwa
serikali kutenga fedha ya usimamizi wa kazi za wasanii. Kikubwa
kinachotakiwa uimarishwe ulinzi wa kazi za wasanii ili waweze kujipatia
maendeleo kupitia kazi zao.
Naye Stara Thomas alisema, “Tumeangaliwa kwa jicho la huruma hivyo tujitambue na tuitumie vyema nafasi hii, pia upande wa wezi wa kazi zetu tutashukuru kama litafanyiwa kazi vizuri kwani wasanii wengi wamekuwa wakikata tamaa kutokana na kuibiwa kazi zao.”
Aidha Mfalme wa Rymes, Afande Sele ameiomba serikali kusimamia na kuhakikisha utekelezaji huo unakamilika na siyo maneno hewa.

Post a Comment