Wanafunzi
316 waliosimamishwa masomo chuo kikuu cha St. Joseph Kampasi ya Dar es
salaam, walifungua kesi ya kuomba kibali cha kuwakilisha wenzao
mahakamani pamoja na chuo kusitisha masomo wakati kesi ya msingi
ikiendelea kusikilizwa.
Kesi hiyo
imetajwa leo June 10 2016 Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam
ambapo imetoa kibali kwa wanafunzi kufungua kesi dhidi ya chuo hicho na
Tume ya vyuo vikuu Tanzania ‘TCU’
Akitoa ufafanuzi wakili wa walalamikaji, Emmanuel Muga amesema……..>>>’hii
kesi ina utaratibu kwa sababu mpo wengi wanafunzi 316 ikiwa ni watu
wengi inabidi upande kibali cha mahakama ili ufungue hiyo kesi na hiyo
kesi itawakilishwa na watu wachache yaani watu wanne tu lakini ili watu
wanne wawakilishe wenzo wote lazima mahakama itoe kibali’
Katika
madai ya msingi, walalamikaji wanadai fidia ya miaka mitatu waliokaa
chuoni hapo dhidi ya chuo na Tume ya vyuo vikuu Tanzania ‘TCU’.
Post a Comment