0
  Afisa mradi wa Bak aids wilayani Liwale bwana Mauridi Mpalama aliyekaa upande wa kulia
                  Mratibu wa Bak aids ngazi ya wilaya bwana Rajib Twalib 

Taasisi inayohusika na kusaidi watoto waishio katika mazingira hatarishi wilayani Liwale mkoanio Lindi ijulikanayo BAK AIDS yasema itajitahidi kuhakikisha inazisaidia kaya hizo za watoto waishio katika mazingira hatarishi na kuwawekea misingi mizuri ili muda wao utakapokwisha bado kuwe na manufaa ya uwepo wao.

Taasisi hiyo iliyochini ya mwamvuli wa baraza la waislam Tanzania Bakwata huku likifadhiliwa na watu wa Marekani lengo likiwa ni kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi yaani pamoja tuwalee.

Akizungumza na Liwale Blog mratibu wa Bak aids ngazi ya wilaya bwana Rajib Twalib amesema taasisi hiyo imeanza kufanya kazi wilayani Liwale tangu machi mwaka 2013 ikishirikiana na serikali za vijiji kwa ajili ya kuwapa walengwa hao,huku akitaja misaada wanayoitoa kuwa ni afya,chakula lishe,elimu,msaada wa ulinzi,malanzi  pamoja na huduma za ukuzaji wa kaya kwa kuunda vikundi vya vikoba kwa ajili ya kujiwekea akiba zitakazowawezesha kukopa na kuanzisha mitaji kwa ajili ya biashara .

Twalib alibainisha kuwa hapa wilayani kuna jumla ya vikundi 74 huku vikundi 50 vikiwa vimesajiliwa na vingine zipo katika hatua za usajili na kusema kuwa watahakikisha kabla ya muda wao kuishia vikundi hivyo vyote vitarasimishwa kwa serikali ili viweze kutambuliwa hata zikitokea taasisi zingine kuja kutoa misaada tayari serikali itakuwa ina watu walio katika vikundi na watu hao kupata misaada kama vile kuwawezesha mikopo ya biashara.

Afisa mradi huo bwana Mauridi Mpalama amesema majukumu yao kama bak aids ni kuhakikisha wanahamasisha walengwa wazazi na walezi wa watoto hao juu ya umuhimu wa vikundi huku akizitaka jamii kuhudumia familia zao,kuwataka wazazi kulea watoto wao huku watoto waliochini ya miaka miaka mitano kuwapeleka watoto wao kliniki na kuzitaka serikali za vijiji wilayani Liwale kutetenga bajeti kwa ajili ya kuwahudumia watoto.

Post a Comment

 
Top