Ziara ya
Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania (Tanzania Saccos for
Women Enterprenuers) imezaa matunda baada ya kikundi hicho cha kina mama
kufanikiwa kuingia mkataba wa ushirikiano (MoU) katika masuala ya
biashara na Kukundi cha Wanawake Wajasiriamali wa Comoro (Association of
Women Entrepreneurs in Comoro).
Makubaliano
hayo ya ushirikiano yalifikiwa kufuatia ziara ya siku mbili iliyofanywa
na Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania nchini Komoro
tarehe 14 Juni 2016. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kutafuta masoko kwa
ajili ya bidhaa za Tanzania nchini Komoro, pamoja na kukutana na
wajasiriamali wa Komoro ili kuweza kubadilishana taarifa juu ya fursa
mbalimbali za biashara kati ya Tanzania na Komoro.
Tukio
hilo la utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano baina ya vikundi
hivyo vya Wajasiriamali akina mama kutoka Tanzania na Komoro
lilishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka F.
Kilumanga. Katika hafla hiyo, Mhe. Balozi Kilumanga aliwapongeza
wajasiriamali hao kwa hatua hiyo muhimu waliofikia na kuwa ana imani
ushirikiano huo utakuwa ni wakudumu na wenye manufaa kwa pande zote
mbili. Alieleza kuwa Tanzania na Komoro zinaweza kushirikiana katika
nyanja mbalimbali za biashara na ana imani kuwa hii itakuwa ni chachu
kwa wawekezaji wengine kutoka Tanzania kuja nchini Komoro kwa ajili ya
kuekeza.
Bi. Naila Thabeet wa Association of Women Enterpreneurs akibadilishana
mkataba na Bi. Anna Matinde kutoka Tanzania Saccoss for Women
Enterprenuers.
Wadua wakishuhudia tukio la kihistoria ambapo ni mara ya kwanza vikundi
vya akina mama kutoka Komoro na Tanzania wamekubaliana kushirikiana
katika nyanja za biashara.
Post a Comment