0
Usalama umeimarishwa nje ya mahakama kuu mjini Nairobi
Wanasiawa 8 nchini Kenya kutoka chama tawala na kile cha upinzani, wamefikishwa mahakamani jijini Nairobi baada ya kukaa kororoni kwa muda wa siku tatu kwa makosa ya kutoa matamshi ya uchochezi.
Waendesha mashtaka amewalaumu kwa kutumia matamshi yanayoweza kusababisha fujo miongoni mwa raia mbali na kudunisha utawala wa taifa.
Video moja iliyowekwa mitandaoni mwishoni mwa juma lililopita, lilimuonyesha mbunge wa chama tawala Jubilee, Moses Kuria, akitoa wito wa kuuawa kwa kinara mkuu wa chama cha upinzani ODM Raila Odinga.
Bwana Kuria amekanusha usemihuo.
Wabunge wengine wa chama tawala wanaokabiliwa na mshtaka hayo ya uchochezi Ferdinand Waititu (Kabete) and Kimani Ngunjiri (Bahati).
Waendesha mashtaka amewalaumu kwa kutumia matamshi yanayoweza kusababisha fujo miongoni mwa raia
Wabunge wa muungano wa upinzani-CORD seneta wa jimbo la Machakos Johnson Muthama wabunge Junet Mohamed (Suna East), Timothy Bosire (Kitutu Masaba), na wawakilishi wa wanawake wa Aisha Jumwa (Kilifi ) na Florence Mutua (Busia ) walijibu matamshi hayo, huku wakiwaomba wafuasi wao kumlinda bwana Odinga.

Post a Comment

 
Top