Usiku wa June 17 2016 klabu ya Dar es
Salaam Young Africans ilitangaza good news kwa mashabiki wake, baada ya
zile tetesi ambazo zilikuwa zimeenea mchana wa siku hiyo, kuthibitika
kuwa ni kweli.
Sasa ni rasmi Yanga imefanikiwa
kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia aliyekuwa
anaichezea klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe Obrey Chirwa kwa mkataba wa
miaka miwili. Ada ya uhamisho Yanga wenyewe hawajaweka wazi ila
soccer24.com walitanga staa huyo kusajili kwa dola 100000 za kimarekani
ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200 za kitanzania.
Orey Chirwa ambaye yupo katika kikosi
cha timu ya taifa ya vijana chini umri wa miaka 23, anakuwa staa wa tatu
kujiunga na Yanga akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, baada ya Donald
Ngoma na Thabani Kamusoko kusajili na wao wakitokea klabu hiyo msimu
uliopita.
Post a Comment