Madawati 30 aliyokabidhi Mfanyabiashara
Haji Mohamedi Lingindo
Mfanyabiashara wa mafuta Wangindo Filling Station wilayani
Liwale mkoa Lindi, Haji Mohamed Lingindo amekabidhi madawati 30 yenye
thamani ya sh. 3,440,000/= kwa mkuu wa wilaya,mhe. Sarah Chiwamba leo septemba 22
katika kuweza kuwasaidia wanafunzi kusomea katika mazingira mazuri.
Aidha Lingindo katika kukabidhi madawati hayo amewataka
wafanyabiashara na wadau wengine wa Liwale kujitokeza kuweza kusaidia jamii kwa
kile kipato wanachopata kwalengo la kuweza kuwasaidia watoto wengine
na vizazi vijavyo waweze kusoma katika mazingira mazuri.
“Mimi ni mmoja wa mdau nilioguswa na uchangiaji wa madawati
kwa Kidogo nilichopata nimeona vema kuisaidia jamii hata vitabu vyetu vya dini
zinasema ukijaliwa kipato tunatakiwa kuisaidia jamii ”alisema Lingindo
Naye mkuu wa wilaya ya
wilaya ya Liwale, mhe. Sarah Chiwamba amesema msaada huo wa madawati ni mfano wa kuigwa na jamii kwani
watoto watakaokalia na kusomea madawati hayo wakiwa madaktari na viongozi
watakumbuka sana msaada huo.
Kaimu afisa elimu shule ya msingi wilaya ya Liwale,Philip
Siyaya amesema anashukuru kwa msaada huo kutoka kwa mfanyabiashara Lingindo na
kuongeza kusema msaada wa madawati hayo atayagawa kwa shule mbili, shule ya
msingi Likongowele na shule ya msingi Kambarage kwakuwa shule hizo zina changamoto
za ongezeko la wahamiaji la wanafunzi ambao wazazi wao wanapohamia Liwale mjini
pamoja na msaada huo kuna madawati ya zaida 517 yaliyohifadhiwa yaliotolewa na ofisi ya
bunge.
Post a Comment