0

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kutaka kuvamia kituo cha Polisi Mzumbe wilaya ya Mvomero ambapo wawili kati yao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya kupigwa risasi na askari wa jeshi hilo wakati wakitaka kutekeleza kosa hilo wakidai polisi kuhusika na kifo cha mtu aliyekuwa ameshikiliwa na hatimaye kuachiwa baada ya kupewa dhamana kisha kufariki dunia akiwa nyumbani kwao.

ITV imefika katika kituo cha Polisi Mzumbe na kukuta wananchi wakiwa wametawanyika huku askari wa jeshi hilo wakiwa wameweka ulinzi mkali katika kituo hicho na hapa kamanda wa polisi mkoani Morogoro Ulrich Matei anathibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Majeruhi wa tukio hilo wanaeleza namna wanavyohusishwa na tukio hilo huku daktari bingwa wa upasuaji wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Francis Semwene akithibitisha kuwapokea majeruhi hao.

Chanzo: ITV

Post a Comment

 
Top